Manifesto Ya Ikolojia Ya Kisasa - Kiswahili
-
-
Share
-
Share via Twitter -
Share via Facebook -
Share via Email
-
Kusema kwamba dunia ni sayari ya binadamu inakuwa kweli kila siku. Binadamu waliumbwa kutoka duniani na dunia huumbwa tena kwa mikono ya wanadamu. Wanasayansi wengi nchini hueleza hii kwa kusema kwamba dunia imeingia mwanzo mpya wa kipindi cha kijiolojia: Anthropocene, umri wa binadamu.
Kama wasomi, wanasayansi, wanaharakati na raia, sisi huandika kwa imani kwamba maarifa na teknolojia ikitumika kwa hekima, huweza kuruhusu umri wa binadamu kwa wema au hata kwa ukubwa. Umri mzuri wa binadamu hudai kwamba binadamu watumie nguvu zao za kijamii, kiuchumi na teknolojia kwa kufanya maisha ya watu bora, utulivu wa hali ya hewa na kulinda dunia ya asili.
Katika hili, sisi huthibitisha moja la muda mrefu, ubora wa mazingira. Kwamba binadamu wanapunguza athari zake za mazingira na kutoa fursa zaidi kwa mambo ya asili. Wakati sisi hukataa lingine, kwamba jamii za kibinadamu lazima zikubaliane na vitu vya asili ili kuepuka kuanguka kwa uchumi na mazingira.
Maadili haya mawili hayawezi tena kuambatishwa. Mifano ya asili sio kama sheria za kawaida, haziwezi kulindwa au kuimarishwa kwa upanuzi wa utegemezi wa binadamu kwa riziki na ustawi wake.
Anthropocene nzuri hudai kufanya maisha ya watu yawe bora zaidi, utulivu wa hali ya hewa na kulinda ya asili kwamba binadamu hutumia ukuaji wa kijamii, dunia kiuchumi na nguvu za kitekinolojia.
Uzidishaji wa shughuli nyingi za binadamu hasa kilimo, uchimbaji nishati, misitu na makazi ili waweze kutumia ardhi ndogo na kulinda ardhi ya asili ni muhimu kwa maendeleo ya binadamu na kuondoa athari za mazingira.
Hizi taratibu za kiuchumi na kijamii na teknolojia ni muhimu katika uchumi wa kisasa na uhifadhi wa mazingira. Pamoja huruhusu watu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira asili na kupunguza umaskini duniani.
Ingawa sisi hadi sasa tumeandika maoni yetu tofauti, yanazidi kujadiliwa kwa ujumla. Sisi wenyewe tunajiita watu wa kisasa na wanavitendo. Tunatoa tamko hili kiithibitisha na kufafanua maoni yetu na kueleza maono yetu kwa ajili ya kuweka nguvu za ajabu za mwanadamu katika huduma ya kujenga ‘Anthropocene’ umri mzuri wa binadamu.
1.
Ubinadamu umestawi zaidi ya karne mbili zilizopita. Wastani wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 30 hadi 70, na kusababisha watu kuongezeka kwa idadi kubwa na uwezo wa kuishi katika mazingira mbalimbali. Ubinadamu umepiga hatua ya ajabu katika kupunguza matukio na athari za magonjwa na umekuwa unastahimili zaidi hali ya hewa na majanga mengi ya asili.
Teknolojia ya binadamu, kutoka enzi za wale ambao ndio wa kwanza kukimudu kilimo na kuchukua nafasi ya uwindaji na kukusanya (matunda) hadi hawa ambao leo wanaendesha uchumi wa kiutandawazi, wamewafanya binadamu wasitegemeee sana mifumo ya ikolojia ambayo hapo awali iliwaletea riziki zao tu, hata ingawa mazingira hayo huachwa yakiwa yameharibika kabisa.
Vurugu za aina zote zimepungua kwa kiasi kikubwa na pengine ni za kiwango cha chini kabisa kilichowahi kushuhudiwa na kiumbe bianadamu, vitisho vya karne ya 20 licha ya ugaidi wa leo.
Kiutandawazi, binadamu wamehama kutoka serikali ya mtu mmoja, (udikteta) kuelekea demokrasia huria inayotawaliwa na kanuni za sheria na uhuru mwingi.
Uhuru wa kibinafsi, kiuchumi na kisiasa umeenea duniani kote na kwa kiasi kikubwa
Kukubalika kama maadili ya watu wote.
Usasa umewaweka wanawake huru kutoka katikamajukumu ya kijinsia ya jadi,nakuongeza udhibitiwa uzazi wao. Kihistoria idadi kubwa ya binadamu - kiasilimia na katika hali halisi - wanausalama na hawaathiriki kutokana na umaskini na utumwa.
Wakati huo huo kustawi kwa wanadamu kumechukua kiwango kizito katika mazingira ya asili, mazingira hasi kwa binadamu na wanyamapori. Binadamu hutumia nusu ya dunia isiyo na barafu, hasa kwa ajili ya malisho, mazao na uzalishaji wa misitu. Katika nchi ambayo hapo mwanzo ilikuwa imefunikwa na misitu asilimia 20 imegeuzwa kwa matumizi ya binadamu. Idadi kubwa ya wanyama wa majini na ndege wamepungua kwa kiasi cha zaidi ya asilimia 50 katika kipindi cha miaka 40 peke yake. Aina zaidi ya 100 ya makundi hayo yalikuwa yametoweka katika karne ya 20, na kiasi cha aina 785 tangu mwaka 1500. Wakati tunavyoandika sasa, ni vifaru weupe wanne tu wa kaskazini waliothibitishwa kuwapo.
Kutokana na hali kwamba binadamu wanategemea kikamilifu Biosfia (sehemu ya dunia yenye uwezekano wa uhai), inawezekanaje watu wanafanya uharibifu mkubwa sana kwa mifumo ya asili bila kujiletea madhara zaidi kwao wenyewe?
Jukumu la teknolojia katika kupunguza utegemezi wa binadamu kwenye mazingira ya asili linaweza kuelezea kitendawili hiki.
Teknolojia ya binadamu, kutoka enzi za wale ambao ndio wa kwanza kukimudu kilimo na kuchukua nafasi ya uwindaji na kukusanya (matunda) hadi hawa ambao leo wanaendesha uchumi wa kiutandawazi, wamewafanya binadamu wasitegemeee sana mifumo ya ikolojia ambayo hapo awali iliwaletea riziki zao tu, hata ingawa mazingira hayo huachwa yakiwa yameharibika kabisa.
Licha ya madai ya msingi ya mara kwa mara kuanzia 1970, “mipaka ya ukuaji” bado kuna ushahidi mdogo sana kwamba idadi ya watu na kupanuka kwa uchumi kunashinda uwezo wa kuzalisha chakula au kupata nyenzo ya rasilimali muhimu katika siku za karibuni.
Kwa kiwango ambacho kuna mipaka halisi iliyowekwa ya matumizi ya binadamu, huwa ni ya kinadharia mno hadi hakuna athari kiutendaji. Kiasi cha mionzi ya jua (sola) inayopiga ulimwengu, kwa mfano, ni mahsusi lakini haiwakilishi kikwazo kikubwa kwa juhudi za binadamu.
Ustaarabu wa binadamu unaweza kustawi kwa karne nyingi na millennia kwa nishati inayotolewa kutoka uranium iliyofungwa au mzunguko wa mafuta ya thorium, au myeyuko wa mchanganyiko haidrojen. Kutokana nausimamizi ufaao, wanadamu hawako katika hatari ya kukosa ardhi ya kutosha ya kilimo kwa ajili ya chakula. Kukiwa na ardhi ya kutosha na kiasi kikubwa cha nishati, pembejeo mbadala huweza kutumiwa kuleta ufanisi wa binadamu ikiwa pembejeo (zakawaida) zinakuwa ghali na haba.
Hata hivyo kunabakia vitisho vikubwa vya muda mrefu vya mazingira kwa ustawi wa binadamu, kama vile mabadiliko ya hali ya hewa ya arithropojenia, utando wa upunguzaji wa stratoferik na utiaji asidi wa bahari. Wakati hatari hizi ni vigumu kuzipima ushahidi wake ni wazi leo kuwa zinaweza kusababisha hatari kubwa ya madhara ya majanga ya mazingira. Hata yale ambayo hayana madhara, yanaweza kuhusishwa na vitisho hivi taratibuna huweza kusababisha gharama kubwa za binadamu na kiuchumi pamoja na kuongezeka kwa hasara za kimazingira.
Sehemu kubwa ya watu duniani bado wanakabialiana na hatari za kiafya za mazingira zaidi ya mara moja.
Ndani nanje uchafu wahewa huendelea kuleta vifo vya mapema na maaradhi kwa mamilioni kila mwaka.Uchafuzi wa maji na magonjwa yanayotokana na maji kutokana na uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji husababisha mambo hayo.
2.
Hata ingawa athari za binadamu katika mazingira zinaendelea kukua mienendo mbalimbali ya muda mrefu leo inaendesha ustawi mkuu wa binadamu kutokana na athari za mazingira.
Kutokana na hali ya sasa, inawezekana kuwa idadi ya binadamu itafikia kilele karne hii kisha ianze kushuka.
Utenganisho unatokea katika masuala yote ya kijamii na ya lazima.
Utenganisho wa kijamii una maana ya kuwa athari za kimazingira kwa mazingira kibinadamu zinaongezekakwa kiwango cha polepole zaidi kuliko ukuaji wa uchumi kwa ujumla. Hivyo, kwa kila kitengo cha pato kiuchumi, chini yaathari ndogo za kimazingira (kwa mfano, uharibifu wa misitu, uharibifu wa fauna-makao ya wanyama mahali, uchafuaji wa hewa) hutokea. Athari za ujumla zinaweza bado kuongezeka, japo kwa kiwango kidogo zaidi kuliko inavyokuwa kwenye masuala mengine.
Utenganisho halisi unatokea wakati athari za kimazingira za jumla - athari za kiwango zinafikia kilele na kuanza kushuka, hata wakati uchumi unaanza kukua.
Utenganisho unaweza kuletwa na yote mawilimienendo ya kiteknolojia na idadi ya watu na kwa kawaida hutokana na yote mawili.
Ongezeko la idadi ya watu tayari linashuhudiwa. Kiwango cha ongezeko hilo la watu hivi leo ni asilimia moja kwa mwaka, kutoka asilimia 2.1 katika miaka ya sabini. Viwango vya uwezo wa uzazi katika nchi zilizo na zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni vimepungua kabisa. Ongezeko la idadi ya watu kimsingi huchangiwa na muda mrefu wa kuishi na viwango vya chini vya vifo, siyo kwa kuongezeka kwa uwezo wa kuzaa. Inavyoelekea, inawezekana kwamba idadi ya watu itafikia upeo wake katika karne hii na kuanza kupungua.
Mielekeo katika idadi ya watu inahusiana na mabadiliko katika maisha na uchumi wa watu hao. Kwa mara ya kwanza katika historia ya binadamu, zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni wanaishi mijini. Kufikia mwaka 2050, inakadiriwa kwamba asilimia 70 ya watu itakuwa ikiishi mijini, idadi ambayo inaweza kuongezeka na kufikia asilimia 80 au zaidi mwisho wa karne hii. Miji ina idadi kubwa ya watu wa viwango vya chini vya uzazi.
Miji huchukua asilimia moja hadi tatu tu ya ardhi ya dunia ilhali ni makao ya takribani bilioni nne ya watu.
Miji huchukua asilimia moja hadi tatu tu ya ardhi ya dunia ilhali ni makao ya takribani bilioni nne ya watu. Hivyo basi, miji huwakilisha na kuendesha jumla ya maisha ya binadamu, kwa kuwawezesha kupata riziki zao vizuri kushinda mashambani huku ikipunguza athari za kimazingira.
Ukuaji wa miji pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kimazingira ambayo hutokana na ukuaji huo haviwezi kutenganishwa na ufanisi wa kilimo. Kwa kuwa kilimo kimeendelea kupanuka, ardhi na kazi kuongezaka idadi kubwa ya watu imehama kutoka mashambani kuelekea mijini. Takribani nusu ya idadi ya watu Marekani walifanya kazi mashambani mwaka wa 1880. Hivi leo, ni chini ya asilimia 2 wafanyao.(kazi hizo)
Kwa kuwa maisha ya binadamu yamewekwa huru dhidi ya kazi ngumu ya kilimo, ni wafanyakazi wengi wamepata uhuru huo pia ili wafanye shughuli nyingine. Miji, wanavyoiona leo, isingekuwepo ila kwa mabadiliko makubwa katika kilimo. Katika hali kinzani, usasa hauwezi kuafikiwa katika kilimo ambacho lengo lake kuu ni kupata chakula.
Maendeleo haya yamepunguza haja ya kuwa na wafanyakazi wengi kwa kila hamba na vilevile kupunguza mahitaji mengi ya shambani. Huu si mkondo mpya: mavuno yamekuwa yakipungua katika milenia kutokana na kupungua kwa kiasi kinachohitajika kumlisha mtu. Kiasi ardhi inayotumika hivi leo ni cha chini kuliko ilivyokuwa miaka 5,000 iliyopita licha ya kuwa watu wa kisasa wana chakula bora. Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia katika kilimo, katika nusu ya karne kuanzia miaka ya kati ya 1960, kiwango cha ardhi inayohitajika kwa upanzi wa mimea na kulisha wanyama kwa binadamu wa kawaida kilipungua kwa nusu.
Makuzi ya kilimo, pamoja na kuachana na matumizi ya kuni kwa upishi, yametoa nafasi kwa kuongezeka kwa misitu katika maeneo mengi ya dunia. Takribani asilimia 80 ya Uingereza ya Sasa hivi ina misitu, ikilinganishwa na takribani asilimia 50 iliyokuwepo mwisho wa karne ya 19. Kwa Zaidi ya miaka 20 iliyopita, kiwango cha ardhi kilichotengewa misitu zalishi ulimwenguni kilipungua kwa hekari milioni 50, eneo linalotoshana nanchi ya Ufaransa. ‘Mabadiliko ya kimisitu’ kutoka kwa ukataji wa misitu hadi katika uongezaji wa misitu yanaonekana kuwa kiashiria kizuri cha maendeleo sawa na ilivyo kwa mabadiliko ya tabia za binadamu inayopunguza idadi ya watu wanaozaliwa kwa kuwa hupunguza umaskini.
Utumiaji wa nyenzo nyingine za maisha ya binadamu pia unaendelea kuongezeka. Kiwango cha maji yanayohitajika kwa matumizi ya kawaida kimepungua kwa takribani asilimia 25 kwa Zaidi ya nusu ya karne iliyopita. Athari za kemikali ya kinitrojeni zinaendelea kusababisha ongezeko la yutrofia na mikingamo mikubwa katika sehemu kama vile ghuba ya Meksiko. Huku kiwango cha athari hiyo ya kinitrojeni kikiendelea kuongezeka, kiwango kinachotumika kwa kila kitengo cha uzalishaji nacho kimepungua katika mataifa yaliyoendelea.
Kwa jumla, mielekeo hii ina maana kwamba athari ya kijumla ya binadamu kwa mazingira, ikiwa ni pamoja mabadiliko katika utumizi wa ardhi, utumizi wa kupita kiasi na uchafuzi wa mazingira, vinaweza kufikia upeo wake na kupungua karne hii. Kwa kuelewa na kukuza shughuli hizi zinazochipuka, binadamu wana nafasi ya kupanua na kuipanda miti tena Duniani – hata kadiri nchi zinazoendelea zinapoendelea kupata maisha ya kisasa, na kumaliza umaskini wa mali.
Kwa kweli, katika hali kinzani, mahitaji ya bidhaa halisi yataendelea kudidimia kadiri jamii inavyokuwa tajiri. Ulaji nyama, kwa mfano, umefikia upeo wake na sasa watu wanaanza kula protini ambazo hazihitaji utumizi mkubwa wa ardhi.
Mahitaji ya bidhaa halisi yanapoendelea kuafikiwa, nchi zilizoendelea hushuhudia viwango vya juu utumiaji pesa kwa huduma zisizohitaji bidhaa nyingi na sekta za kielimu, hali inayoashiria kwamba shughuli za kiuchumi zinaanza kusambazika. Mageuzi haya yanaweza kuwa hata Zaidi katika nchi zinazoendelea kwa sasa, ambazo huenda zikanufaika kutokana na kuchelewa kuyakaribisha mabadiliko hayo ya kiteknolojia.
Kwa jumla, mielekeo hii ina maana kwamba athari ya kijumla ya binadamu kwa mazingira, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika utumizi wa ardhi, utumizi wa kupita kiasi na uchafuzi wa mazingira, vinaweza kufikia upeo wake na kupungua karne hii. Kwa kuelewa na kukuza na shughuli hizi zinazochipuka, binadamu wana nafasi ya kupanua na kuipanda miti tena Duniani – hata kadiri nchi zinazoendelea zinapoendelea kupata maisha ya kisasa, kumaliza umaskini wa mali.
3.
Michakato ya kupunguza changamoto iliyoelezwa hapo juu kuwa jamii za awali za binadamu ziliishi sana ardhini kushinda ilivyo kwa jamii za sasa. Kwamba jamii za awali zilikuwa na athari ndogo kwa mazingira, ilikuwa ni kwa sababu jamii hizo zilihimiza sana idadi ndogo ya watu.
Teknolojia zilizotumiwa na wahenga wa jamii za binadamu kuafikia mahitaji yao ya kila siku zilihimiza viwango vya chini vya maisha huku pakiwa na nafasi kubwa ya athari kwa mazingira.
Kwa kweli, binadamu walioishi awali ambao hawakuwa na teknolojia zilizoimarika walikuwa na mtagusano wa karibu sana na ardhi kushinda jamii za hivi leo. Izingatiwe kwamba Wamarekani wa Kaskazini milioni moja au mbili waliwinda wanyama wakubwa wakubwa barani humo hata wakaisha katika miaka ya Pleistocene, huku wakichoma na kukata misitu ya barani humo katika mchakato huo. Mabadiliko makubwa katika mazingira yaliyoletwa na binadamu katika kipindi kizima cha Helocene: hivi kwamba zaidi ya robo tatu ya ukataji wa misitu ulimwenguni ulifanyika kabla ya kipindi cha Mabadiliko ya Kiviwanda.
Teknolojia zilizotumiwa na wahenga wa jamii za binadamu kuafikia mahitaji yao ya kila siku zilihimiza viwango vya chini vya maisha huku pakiwa na nafasi kubwa ya athari kwa mazingira. Hatua yoyote ya kujaribu kurudisha jamii hizi za kibinadamu katika uhusiano wake na mazingira asili kwa kutumia teknolojia hizi inaweza kusababisha majanga yasiyotarajiwa.
Makazi ya wanyama duniani kote yako katika hatari hivi leo kwa sababu watu huyategemea kupita kiasi: watu wanaotegemea kuni na makaa hukata na kupunguza misitu; watu wanaokula wanyama wa kuwinda huwapunguza wanyama hata wengine wakaisha. Iwe ni jamii ya wenyeji au mashirika ya asili ya kigeni yanayonufaika, ni utegemezi wa binadamu kwa mazingira asili ambao ni tatizo kwa utunzaji wa mazingira asilia.
Kinyume cha hayo, teknolojia za kisasa, kwa kutumia mazingira asilia, hutiririka vizuri na kufanya kazi vizuri, kutoa nafasi ya kupunguza uharibifu wa binadamu kwa mazingira. Kuzikaribisha teknolojia hizi ni hatua nzuri katika kuafikia mazingira ya kufaa.
Michakato ya kuleta usasa ambayo imeendelea kumuweka binadamu huru dhidi mazingira asili bila shaka ina pande mbili kwa kuwa imesababisha vilevile uharibifu wa mazingira asili. Fueli za visukuku, utumizi wa mashine na shughuli za kiviwanda, mbolea zinazotokana na nyuzi na dawa za kuua wadudu, utumizi wa umeme na teknolojia za uchukuzi na mawasiliano, kwanza zimepanua idadi ya watu na kuwezesha utumizi wa vitu kupanuka vilevile. Teknolojia zingekosa kuimarika kutoka siku za awali, bila shaka idadi ya watu isingeongezeka ilivyoongezeka.
Aidha, ni kweli kwamba idadi kubwa ya wakazi mijini imeweka shinikizo kubwa kwa mazingira asili yaliyo katika sehemu za mbali – utoaji wa maliasili umepanuka. Lakini tena teknolojia hizo zimewawezesha watu kupata chakula, makazi, joto, mwangaza, na kuweza kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine kupitia kwa njia ambazo haziharibu mali asili kama ilivyowahi kuwa katika kipindi kingine chochote cha historia ya binadamu.
Kuyatenganisha maisha ya binadamu na uharibifu wa mazingira kunahitaji michakato kamambe ya kufanya hivyo. Katika visa vingine, lengo huwa ni kutoa vibadala vya kiteknolojia. Kupunguza ukataji miti na uchafuzi wa mazingira ya ndani ya nyumba kunahitaji kutoa kibadala cha kuni na makaa kama njia mpya ya kupata kawi.
Ukuzaji miji, ukuzaji maji, ukuzaji wa kilimo, kawi ya kinyuklia, na upunguzaji chumvi, yote ni michakato ambayo imethibitika kuweza kupunguza haja za kimazingira, hivi kutoa nafasi ya kupatikana na viumbe vingine visivyo binadamu.
Katika visa vingine, lengo la ubinadamu linapaswa kuwa mali asili katika njia stahifu. Kwa mfano, kuongeza mazao ya kilimo kunaweza kupunguza ubadilishwaji wa misitu kuwa mashamba ya kilimo. Binadamu wanapaswa kujitahidi kuyaweka mazingira huru dhidi ya uchumi.
Ukuzaji miji, ukuzaji maji, ukuzaji wa kilimo, kawi ya kinyuklia, na upunguzaji chumvi, yote ni michakato ambayo imethibitika kuweza kupunguza haja za kimazingira, hivi kutoa nafasi ya kupatikana na viumbe vingine visivyo binadamu. Kupunguza miji, kilimo cha mazao ya kiwango kidogo, na njia nyingine nyingi za uzalishaji wa kawi inayoweza kutengenezwa tena, kinyume na matarajio, kwa jumla huhitaji ardhi na raslimali zaidi na hivyo kuacha nafasi finyu sana kwa uasili.
Mikondo hii inaashiria kuwa binadamu wana uwezo wa kutoharibu uasili kwa sababu huo uasili hauhitajiki kuwapa mahitaji yao bali wayaache mazingira hayo huru kwa sababu za kiujumi na kiimani. Sehemu za dunia hii ambazo hazijaguswa ziko hivyo kwa sababu binadamu hajapata haja ya kiuchumi katika sehemu hizo – milima, majangwa, misitu ya majini, na ardhi nyingine ‘duni’.
Utenganishaji hutoa uwezekano kwamba jamii zinaweza kuafikia upeo wa athari za kibinadamu bila kuingilia zaidi sehemu zisizopaswa kuguswa. Uasili usiotumika ni uasili uliotunzwa.
4.
Uafikiaji wa kutosha kwa kawi ya kisasa ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya binadamu na katika kutenganisha maendeleo na uasili. Uwepo wa kawi nafuu huwapa watu ulimwenguni fursa ya kuacha kutumia misitu kama nishati (fueli). Huwapa binadamu fursa ya kupanda vyakula zaidi katika sehemu ndogo ya ardhi, kutokana na mbolea na matrekta yanayotengenezwa kwa kutumia kawi ya kiteknolojia. Kawi huwawezesha binadamu kutumikisha maji yaliyokwisha kutumiwa na kuondoa chumvi katika maji ya bahari ili kuokoa mito na vyanzo vya maji. Huwawezesha binadamu kutumikisha tena vyuma na plastiki badala ya kuchimbua madini. Katika siku za baadaye, kawi ya kisasa inaweza kutoa nafasi ya kunasa kwa kaboni kutoka angani ili kupunguza kaboni ambayo husababisha ongezeko la joto.
Uafikiaji wa kutosha kwa kawi ya kisasa ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya binadamu na katika kutenganisha maendeleo na uasili.
Hata hivyo, kwa angalau karne tatu zilizopita, ongezeko katika uzalishaji wa kawi ulimwenguni limekwenda sambamba na ongezeko la hewa kabonidioksidi. Mataifa vilevile yamechukua hatua ya kupunguza kaboni ingawa kwa kiwango cha chini – yaani, kupunguza viwango vya kaboni katika mataifa hayo – kwa kipindi hicho cha wakati. Lakini hayajawa yakifanya hivyo kwa kiwango kinacholingana na kile kinachoweza kupunguza kaboni inayotolewa hivi kwamba ingekuwa chini ya ile inayotambulika katika ngazi za kimataifa ya digrii 2 za joto ulimwenguni. Katika hatua ya kukabili hali hii ya joto, hivyo basi, itahitaji kwamba binadamu waongeze hatua zilizopo za kupambana na kaboni.
Kuna mkanganyo hata hivyo, kuhusiana na jinsi hili litakavyokabiliwa. Katika nchi zinazoendelea, ongezeko katika matumizi ya kawi linakwenda sambamba na ongezeko katika mapato na uimarikaji wa viwango vya maisha. Ingawa utumizi wa nyenzo nyingine asilia kama vile nitrojeni, mbao na ardhi umeanza kuimarika, Ukuu wa kawi katika maendeleo ya binadamu na matumizi yake mengi kama kibadala cha bidhaa na mali za kutumiwa na binadamu zinaashiria kwamba utumizi wa kawi utaendelea kuongezeka katika karne ya 21.
Kwa sababu hiyo, mgongano wowote kati ya hatua za kukabili ongezeko la joto na michakato ya maendeleo ambayo inawawezesha mabilioni ya watu duniani kuboresha maisha yao, utatatuliwa kwa manufaa ya michakato hii ya maendeleo.
Mabadiliko katika hali ya anga na changamoto nyingine za kimazingira siyo masuala ya kimsingi yanayopaswa kuwashughulisha watu wengi duniani. Na wala hazipaswi kuwa. Kituo kipya cha madini ya makaa nchini Bangladesh kinaweza kusababisha uchafuzi wa hewa na ongezeko la kabonidioksidi lakini kitaokoa maisha vilevile. Kwa mamilioni ya watu wanaoishi bila mwangaza na ambao hulazimika kuchoma samadi kupika chakula chao, kupata umeme na fueli za kisasa, hata zikitoka wapi, huwasaidia kupata maisha bora hata kama zina changamoto nyingine za kimazingira.
Hatua kamambe za kukabili mabadiliko kati hali ya joto kimsingi ni changamoto ya kiteknolojia. Hivi tunamaanisha kwamba hata mabadiliko ya aina gani katika utumizi wa kiuchumi ulimwenguni hautatosha kukabili vya kutosha mabadiliko haya katika hali ya joto. Bila ya teknolojia mwafaka hakutakuwa na mikakati ya kukabili ongezeko hili la joto. Japo wanateknolojia hutofautiana kuhusu mbinu mbalimbali za kiteknolojia wanazopendelea, hatujui hatua yoyote ya kukabili ongezeko la joto ambapo mabadiliko ya kiteknolojia hayachangii kupungua kwa joto hilo linalotolewa.
Mbinu maalumu za kiteknolojia ambazo watu wanaweza kufuata katika kukabili suala la joto bado linajadiliwa. Nadharia zinazohusiana na jinsi ya kukabili zinaakisi mapendeleo ya kiteknolojia ya waanzilishi wake na tathmini zinazotolewa huku zote mara kwa mara zikishindwa kushughulikia masuala ya gharama, kiwango na vipimo vinavyoweza kutumikishwa kupata teknolojia ya kaboni ya chini.
Ili kuhamia katika ulimwengu ambao kawi inayotumiwa haitakuwa na kaboni kutahitaji tekonolojia za kawi ambazo zina uzito wa nguvu na zilizo na uwezo wa kuzalisha makumi ya terawati ili kuafiki viwango vya kawi ya kutumiwa katika kuendesha uchumi wa binadamu.
Historia ya mabadiliko ya kawi, hata hivyo, inapendekeza kuwa kumekuwa na mikondo fulani inayohusishwa na mbinu mbalimbali ambazo jamii hutumia kuafikia kawi safi. Kubadilisha fueli ya ubora wa juu (k.v. iliyo na kaboni ndogo, iliyo na uzito wa juu) na ile ya ubora wa chini (k.v. iliyo na kaboni nyingi, uzito wa chini) mara moja ni njia mojawapo wa jinsi jamii imepunguza kaboni, inaelekeza katika njia bora za kukabiliana na kaboni katika siku zijazo. Kuhamia katika ulimwengu ambao kawi inayotumiwa haitakuwa na kaboni kutahitaji tekonolojia za kawi ambazo zina uzito wa nguvu na zilizo na uwezo wa kuzalisha makumi ya terawati ili kuafiki viwango vya kawi ya kutumiwa katika kuendesha uchumi wa binadamu.
Aina nyingi za kawi inayoweza kuzalishwa upya kwa bahati mbaya, haziwezi kufanya hivyo. Viwango vya utumizi wa ardhi na athari nyingine kwa mazingira zinazohitajika ili kupata kawi duniani kutokana na fueli za kimazingira au nyingine nyingi ambazo ni za kuzalishwa upya zina sifa ya kuelekeza kuondoa kaboni.
Seli faafu zinazotengenezwa ardhini kutokana na jua ni tofauti na zina uwezo wa kutoa makumi mengi ya terawato kwenye asilimia ndogo ya ardhi ya Dunia. Teknolojia za kisasa za kawi inayotokana na jua zinahitaji ubunifu wa kutosha kuafikia viwango na ujenzi wa teknolojia za kuhifadhi kawi hiyo ambazo ni nafuu na ambazo zinaweza kukabiliana na aina mbalimbali za kawi katika viwango vya juu.
Mgawanyo wa nyuklia hivi leo ndio teknolojia ya kipekee isiyo na kaboni na iliyo na uwezo wa kuafikia mahitaji mengi ya kawi katika uchumi wa sasa. Hata hivyo, changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi, na kiasasi huufanya utumizi huu wa teknolojia za kinyuklia kutoweza kukabiliana na tatizo hilo la ongezeko la joto. Kizazi kipya cha teknolojia za kinyuklia ambazo ni salama na nafuu kitahitajika ndipo kawi kinyuklia iweze kuafikia uwezo wake kamili kama teknolojia kamambe ya kukabili mabadiliko ya halijoto.
Hatimaye, kizazi kijacho cha kawi inayotokana na jua, mgawanyo imara wa kinyuklia, na muungano wa nyuklia ni njia zinazopigiwa upatu katika njia hitajika za kuimarisha halijoto na kutenganisha binadamu na uasili wa kimazingira. Ikiwa historia ya mabadiliko ya kawi, inaweza kurejelewa kama mfano, hata hivyo, mabadiliko hayo yatachukua muda. Katika kipindi hicho cha mabadiliko, teknolojia nyingine za kawi zinaweza kutoa manufaa mengine ya kiuchumi na kimazingira. Vidimbwi vya maji vinavyotumiwa katika uzalishaji wa kawi, kwa mfano, inaweza kuwa njia nafuu ya kutengeneza kawi ya kutumiwa nyumbani iliyo na kaboni ndogo kwa mataifa maskini ingawa ardhi na vitovu vyao vya maji huwa vikubwa. Fueli za visukuku zilizo na uwezo wa kunasa na kuhifadhi kaboni vinaweza kutoa manufaa machache ya kimazingira dhidi ya kawi zinazotokana na visukuku au samadi.
Njia bora na ya kipragmatiki katika kuafikia uchumi ulio na kawi ya kudumu na bora huhitaji kwamba binadamu wabadilike haraka iwezekanavyo na kuanza kutumia kawi ambazo ni nafuu, safi, nzito, na zilizoko kwa wingi.
Njia bora na ya kipragmatiki katika kuafikia uchumi ulio na kawi ya kudumu na bora huhitaji kwamba binadamu wabadilike haraka iwezekanavyo na kuanza kutumia kawi ambazo ni nafuu, safi, nzitp, na zilizoko kwa wingi. Njia kama hiyo itahitaji kujitolea kwa umma kuchangia katika maendeleo hayo na ujenzi wa teknolojia zenye kawi safi, katika mataifa husika na miongoni mwao, kupitia kwa ushirikiano na ushindani wa kimataifa, na katika mfumo mpana wa usasa utandaridhi na maendeleo.
5.
Tunaandika kijitabu hiki kama wapenzi na wahusika wa dhati kwa uasili wa kimazingira. Kwa kutambua, kuchunguza, kutafuta kuelewa, na kutalii uasili wa kimazingira, watu hujitolea wakatoka katika mipaka yao. Hujiunganisha na historia ya kindani ya mabadiliko yao. Hata pale watu hawaingiliani moja kwa moja na uasili huu wa kimazingira, husisitiza uwepo wake kama kitu muhimu kwa maisha yao kisaikolojia na kiimani.
Tunaandika kijitabu hiki kama wapenzi na wahusika wa dhati kwa uasili wa kimazingira.
Binadamu hutegemea uasili kwa kiwango fulani kila mara. Hata ikiwa ulimwengu ambao umeshikamana kikamilifu ungekuwepo, wengi wetu tungeteua kuishi kwa kuhusiana kwa karibu na uasili wa kimazingira kushinda inavyohitajika kwa teknolojia na utunzaji wa binadamu. Utenganishaji hutoa nafasi ya kutambua uwezekano kwamba utegemezi wa binadamu kwa bidhaa usiwe na hasara au madhara makubwa.
Hali hai, ya kinadhiri, na iliyoimarika ya utenganishaji wa binadamu na shughuli zake na uasili ili kutunza uasili wa kimazingira ni zao la kiimani na kiujumi kuliko ilivyo kwa hoja zinazojiegemeza kwenye bidhaa na vyombo vya kutumia. Vizazi vya sasa na vijavyo vinaweza kuishi na kujiendeleza kinyenzo katika sayari iliyo na uasili finyu wa kimazingira na mazingira ya pori. Lakini huu si ulimwengu tunaoutaka wala, ikiwa binadamu watakubaliana na utenganishaji huo, wanaweza kuukubali.
Tunachokiita hapa kama uasili wa kimazingira, au hata mazingira pori, ni jumla ardhi ya nchi kavu, maji, na makazi ya wanyama, ndege na wadudu ambayo mara nyingi yamekuwa yakiharibiwa na binadamu kwa karne na milenia. Sayansi ya utunzaji, na dhana za upana wa mazingira, uchangamano, na uasili ni muhimu, lakini wenyewe hawawezi kubaini ardhi za kutunza, au jinsi ya kuzitunza.
Katika visa vingi, hakuna msingi wowote wa awali kabla ya kubadilika kwa binadamu ambapo uasili wa kimazingira unaweza kurudishwa. Kwa mfano, majaribio ya kufufua sura ya ardhi ili zifanane na hali za awali (“uasilia”) inaweza kujumuisha kuondoa viumbe vilivyozuka majuzi (“vizuka”) na hivyo kuhitaji upunguzaji wa mazingira asilia. Katika visa vingine, jamii zinaweza kuamua kuharibu uasilia ili kupata upya.
Pamoja na utenganishaji wa mahitaji ya binadamu dhidi ya uasili wa mazingira, kujenga mikakati kamambe ya kujitolea kutunza pori, mazingira, hali nzuri za mazingira utahitaji uhusiano wa dhati na uasili huo wa mazingira.
Hatua za wazi za kutunza mazingira dhidi ya kuharibiwa kwa kukosa matumizi yasiyofaa ni hatua za kianthropojenia. Kwa sababu hii, hatua zote za kuyatunza ni za kianthropojenia. Utenganishaji wa mazingira pori ni teuo la kibinadamu, kwa huduma za mapenzi ya binadamu, kushinda kuilazimisha. Binadamu watahifadhi maeneo pori na mazingira kwa kuwasadikisha raia wenzetu kwamba maeneo haya, na viumbe vilivyomo, ni muhimu kutunzwa. Watu wanaweza kuamua kuwa na huduma nyingine – kama usafishaji wa maji na ukingaji dhidi ya mafuriko – alimuradi wanatumia mifumo asilia, kama vile vyanzo vya maji misituni, miamba, na maeneo yenye unyevu, hata kama mifumo hiyo asilia ni ghali kushinda kujenga vituo vya kutibu maji, na kingo za kuzuia maji. Hakuwezi kuwa na moja inayoafiki kila sehemu.
Mazingira yataboreshwa na mapendeleo mbalimbali ya kimaeneo husika, kihistoria na kitamaduni. Huku tukiamini kwamba maendeleo ya kilimo kwa utunzaji wa ardhi ni muhimu katika kutunza mazingira pori, tunatambua kwamba jamii nyingi zitaendelea kupendelea utumiaji ardhi, huku wakiazmia kutunza wanyama pori waliomo katika mashamba ya kilimo, kwa mfano, badala ya kurudia mazingira pori, nyasi, vichaka na misitu. Pale ambapo utenganishaji unapunguza shinikizo kwenye ardhi na makazi ya wanyama kuafikia mahitaji ya kimsingi ya binadamu, wamiliki wa ardhi, jamii, na serikali lazima ziamue ikiwa ardhi hiyo inatengwa kwa ajili ya kiujumi au kiuchumi.
Utenganishaji pekee hautatosha kuhakikisha mazingira pori. Ni lazima kuwe siasa za utunzaji na vuguvugu la kutunza mazingira pori ili kutetea kuhifadhiwa zaidi kwa mazingira pori kwa sababu za kiujumi au kiimani. Pamoja na utenganishaji wa mahitaji ya binadamu dhidi ya uasili wa mazingira, kujenga mikakati kamambe ya kujitolea kutunza pori, mazingira, hali nzuri za mazingira utahitaji uhusiano wa dhati na uasili huo wa mazingira.
6.
Tunasisitiza haja na uwezo wa kibinadamu wa kuharakisha, kuhaisha na kupanua utenganishaji. Maendeleo ya kiteknolojia hayahitajiki. Utenganishaji wa athari za kimazingira kutokana na vitomeo vya kiuchumi si jukumu ubunifu unaoelekezwa na haja ya soko na haja ya kukidhi kutokuwepo kwa kitu. Ukingo mrefu wa mabadiliko ya binadamu ya mazingira asilia kupitia kwa teknolojia ulianza mapema kabla ya chochote kinachohusiana na soko au bei. Kutokana na haja inayoendelea, ukosefu wa vitu, na kubahatisha ugunduzi, binadamu wameiumba upya dunia kwa milenia.
Masuluhisho ya kiteknolojia kwa matatizo ya kimazingira yanapaswa vilevile kuangaziwa katika mazingira mapana ya kijamii, kiuchumi, na muktadha wa kisiasa. Tunafikiri ni hatua mbaya kwa mataifa kama Ujerumani na Ujapani, na majimbo kama California, kupinga viwanda vya kawi ya kinyuklia, kurudisha kaboni katika sekta zake za kawi, na kuongeza utumizi wa fueli ya kisukuku na bayomasi. Hata hivyo, mifano kama hiyo inaelekeza wazi kwamba teuo za kiteknolojia hazitafanywa na mashirika ya kimataifa bali asasi na tamaduni za kitaifa na za maeneo husika.
Mara kwa mara, usasa umekanganywa na, watetezi na wahakiki wake, pamoja na ubepari, mamlaka ya mashirika, na sera shirikishi. Tunakataa hali kama hizo. Tunachokirejelea tunapozungumza kuhusu usasa ni mabadiliko ya kudumu ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, na kiteknolojia katika jamii za binadamu katika hatua ya kutafuta uhuru wa kibidhaa, afya ya umma, uzalishaji nyenzo, uunganikaji wa kiuchumi, miundombinu imara na uhuru wa kibinafsi.
Usasa umewaweka huru watu wengi dhidi ya maisha ya umaskini na kazi ngumu za kilimo, wanawake kutoka katika matabaka ya kuhamishika, watoto, na makundi tengwa dhidi ya utesi, na jamii dhidi ya serikali geugeu. Uzalishaji nyenzo mkubwa unaohusishwa na mifumo ya teknolojia ya kijamii imetoa fursa kwa jamii za kibinadamu kuafikia mahitaji ya kibinadamu kwa kutumia nyenzo chache na athari ndogo kwa mazingira. Nchi zilizo na uzalishaji mkubwa wa mali ni nchi tajiri, zilizo na uwezo wa kuafikia mahitaji ya kimsingi ya kibinadamu huku ziada yao ya kiuchumi ikiwekezwa katika shughuli nyingi zisizo za kiuchumi, zikiwa ni pamoja na afya ya binadamu, uhuru mkubwa wa kibinadamu na nafasi kubwa kwa binadamu, Sanaa, utamaduni na utunzaji wa uasili wa mazingira.
Utenganishaji wa shughuli za kibinidamu na athari za kimazingira utahitaji kujitolea vilivyo katika maendeleo ya kiteknolojia na mabadiliko ya mara kwa mara ya kijamii, kiuchumi, asasi za kisiasa pamoja na mabadiliko hayo.
Michakato ya usasaishi haijakamilika, hata katika nchi zilizoendelea kiuchumi. Utumizi wa nyenzo umeanza kuimarika katika jamii tajiri. Utenganishaji wa shughuli za kibinidamu na athari za kimazingira utahitaji kujitolea vilivyo katika maendeleo ya kiteknolojia na mabadiliko ya mara kwa mara ya kijamii, kiuchumi, asasi za kisiasa pamoja na mabadiliko hayo.
Maendeleo yaliyoimarika ya kiteknolojia yatahitaji ushiriki hai, kakamavu, na thabiti wa wajasiriamali wa sekta za kibinafsi, masoko, mashirika ya kijamii, na serikali. Japo tunapinga uongo wa ruwaza ya miaka ya 1950, tunaendelea kukubaliana na jukumu kuu la umma katika kukabiliana na matatizo ya kimazingira na kuimarisha ubunifu wa kiteknolojia, ikiwa ni pamoja na utafiti wa kujenga teknolojia bora, kupunguza gharama, na hatua nyingine za kusaidia kuwaleta katika masoko, na kanuni za kudhibiti hatari za kimazingira. Na uhusika wa mashirika ya kimataifa kuhusiana na ubunifu wa kiteknolojia na uhawilishaji wa teknolojia ni muhimu katika sekta za kilimo na kawi.
7.
Tunatoa kauli hii kwa imani kwamba ufanisi wa binadamu na sayari salama kimazingira si jambo linalowezekana bali ni vitu usivyoweza kutenganisha. Kwa kujitolea kwa michakato halisi, inayoendelea, ambayo imeanza kutumikishwa katika kutenganisha maisha ya binadamu dhidi ya uharibifu wa mazingira, tunaamini kwamba maisha hayo ya mbeleni yanaweza kuafikiwa. Kwa hivyo, tunakubaliana na hatua yoyote yenye matumaini ya kutumikisha uwezo wa binadamu na maisha ya baadaye.
Tunathamini kanuni karimu za demokrasia, ustahamilivu, na wingi wazo, hata tunapozisisitiza kama funguo za kuafikia Anthropocene bora.
Tunatumai kwamba kijitabu hiki kinaweza kuchangia katika uimarishaji wa ubora na sauti ya mazungumzo kuhusu jinsi ya kutunza mazingira katika karne ya 21. Mijadala ya mara kwa mara kuhusu mazingira yametawaliwa na misimamo mikali ya pande zote, na kuathiriwa mfumo wa kiimani kanisani, hali ambayo hatimaye huchochea kutostahimiliana. Tunathamini kanuni karimu za demokrasia, ustahamilivu, na wingi wazo, hata tunapozisisitiza kama funguo za kuafikia Anthropocene bora. Tunatumai kuwa kauli hii itayakuza mazungumzo kuhusu njia bora za kuafikia thamani halisi ya binadamu kuhusiana na mazingira na sayari hii bora.
Translated by James Kanuri.